Jumla ya vitambulisho 431 vimetolewa kwa wajasiliamali waliopo maeneo ya mgodi wa dhahabu wa Bingwa kata ya Lwamgasa Mkoani Geita.
Zoezi la uhamasishaji na utoaji wa vitambulisho limeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, baada ya kufanya ziara katika mgodi huo akiambatana na baadhi ya wakuu wa Idara akiwemo kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Donald Nssoko.
Akizungumza na wajasiliamali hao Mhandisi Robart amesema kitambulisho hicho ni mkombozi kwa wanyonge pia kitawasaidia wachimbaji wadogo kutambulika kirahisi na kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Aidha amewataka waajiri wote wa migodi kutoa mikataba kwa waajiriwa wao ili kudhibiti dhuruma na uonevu, hata hivyo amewaasa kuepuka kutoa ajira kwa watoto wadogo.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Donald Nssoko amesema zoezi la uhamasishaji na utoaji wa vitambulisho litaendelea kufanyika kwenye maeneo mengine ya Wilaya, hivyo wajasiliamali wahakikishe wanapata vitambulisho kwa manuafaa zaidi.
Nae Mkurugenzi wa mgodi wa Bingwa Mwananyanzala aliwahamasisha wamiliki wenzie wa mashimo ya dhahabu, kuwanunulia vitambulisho waajiriwa wao jambo ambalo lilipelekea kila mmiliki kufanya hivyo na kusababisha kati ya vitambulisho 431 vilivyotolewa, vitambulisho 360 vilichukuliwa na wachimbaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa