MRADI WA TASAF II
MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI
Mratibu Gabriel Evarist
1.UTANGULIZI:
Halmashauri ya wilaya Geita ni moja kati ya Halmashauri za Tanzania zilizochaguliwa kuingia kwenye mradi wa TASAF III kwenye wave ya tano. Halmashauri hii ni moja kati ya Halmashauri 6 zinazounda mkoa wa Geita. Halmashauri imegawanyika katika tarafa 4 za Bugando, Kasamwa, Busanda na Butundwe. Kuna jumla ya kata 37, vijiji 145 na vitongoji 626.
Mradi wa TASAF III ulizinduliwa Tanzania Agosti 2012 Mkoa wa Dodoma na Rais wa awamu ya nne Dr Jakaya Mrisho Kikwete. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ulitambulishwa na kuzinduliwa rasmi Januari 2015. Kati ya vijiji 145 vya halmashauri yetu ni vijiji 94 ndio vinavyonufaika na Mapango wa Kunusuru kaya masikini wa TASAF III. Vijiji 51 vilivyosalia viliwasilishwa TASAF Makao makuu kwa lengo la kuviingiza kwenye Mpango.
2.MAFUNZO YALIOTOLEWA.
2.1 KUBAINI WALENGWA
Mafunzo haya yalitolewa ngazi ya wilaya na vijiji vilivyomo kwenye mpango kwa lengo la kuwajengea uwezo wadau wote kuuelewa mradi wenyewe, walengwa wa mradi, sifa za walengwa, manufaa ya mpango kwa jamii na wilaya nzima.
Idadi ya wajumbe waliojengewa uwezo ngazi ya wilaya:-
Mkuu wa wilaya ya Geita 1,Madiwani 46, Timu ya Usimamizi Halmashauri ya Wilaya ya Geita 20,Waandishi wa Habari 6 na wawezeshaji TASAF 66.
Idadi ya wajumbe waliopewa mafunzo ngazi ya vijiji vilivyomo kwenye mpango.
Wenyeviti wa vijiji 94,Halmashauri za vijiji 282 na wakusanya takwimu 334
2.2 KUHAKIKI WA KAYA MASIKINI:
Mafunzo ya kuhakiki kaya masikini yalitolewa kwa lengo la kwenda kukusanya takwimu halisi za kaya ambazo majina yake yalirudi kutoka TASAF Makao Makuu na kugawa vitambulisho vya muda kwa kila mlengwa. Pia kuingiza majina ya watoto wanastahili kusoma shule na kupata huduma ya kliniki kwenye mpango na orodha maalum.
Mafunzo ya uhakiki wa kaya masikini wajumbe waliopewa mafunzo walikuwa kama ifuatavyo:-
Wawezeshaji TASAF 66,Walimu shule za msingi na sekondari 187,wahudumu wa afya 93, wakusanya takwimu 287,watendaji wa vijiji 94, wenyeviti wa vijiji 94 na Halmashauri za vijiji 282
2.3 KUFANYA MALIPO.
Mafunzo ya kufanya malipo yalitolewa kwa wawezeshaji wa ngazi ya wilaya na wadau wote vijijini. Kamati za kusimamia mpango wa TASAF ngazi za vijiji zilipewa majukumu ya kila mjumbe kwenye kamati hiyo kwa kuwabainisha wahasibu, watunza kalenda, watakaohusika nafomu za utimizaji wa masharti na watakao shughulika na walengwa.
Pia watoa huduma za afya na walimu walipewa mafunzo ya ujazaji wa fomu za utimizaji wa masharti ya elimu na afya pindi zitakapo wafikia kwenye vituo vyao. Idadi ya wajumbe waliopewa mafunzo nikama ifuatavyo:-
Wawezeshaji TASAF 66,Kamati za mradi vijijini 1316,Walimu msingi na Sekondari 187, Wahudumu wa afya 94, watendaji wa vijiji 94 na Halmashauri za vijiji 282.
3.SHUGHULI ZILIZOFANYIKA.
2:1 UTAMBUZI WA KAYA MASIKINI
Shughuli Utambuzi wa kaya ilifanyika kwa siku zisizopungua nne kwa kila kijiji kilichopo kwenye mpango. Shughuli hii ilifanywa na wawezeshaji kutoka ngazi ya Wilaya kwa usimamizi wa Mtaalam Mshauri (TA) na wawezeshaji ngazi ya Taifa.
Wawezeshaji walikuwa na jukumu la kuutambulisha mradi wa TASAF III wa Mpango wa kunusuru kaya masikini kwenye mikutano ya ndani kwa viongozi wa vijiji, Halmashauri za viijiji na mikutano ya hadhara kwa wanavijiji wenyewe kwa vijiji vyote 94. Lengo likiwa ni kuelezea dhima nzima ya mradi, lengo la mradi, walengwa wa mradi, vigezo vya kuwa mlengwa wa mradi na pia zoezi zima la kuwapata walengwa wa mradi ambazo zilikuwa ni kaya masikini sana na hasa zenye watoto.
zenye sifa zifuatazo:-.
Sifa za kaya masikini zilikuwa ni pamoja na:-
•Kaya zisizopata walau mlo mmja kwa siku.
•Kaya zisizokuwa na uweao wa kupata mavazi bora.
•Kaya zisokuwa na kipato chakutegemewa.
•Kaya zisizokuwa na uwezo wa kupeleka watoto shule.
•Kaya zisizoweza kumudu gharama za matibabu.
Zoezi hilo lilifanyika kwa wawezeshaji kwa kushirikiana na vijana waliochaguliwa kwa kila kijiji kuzidodosa kaya hizo kwa kuzingatia vigezo vya umaskini vilivyowekwa katika madodoso maalum yaliyoandaliwa kutoka TASAF Makao Makuu na vigezo vingine vilitokana na mikutano ya hadhara ya wanajamii kijijini hapo. Katika zoezi hili jumla ya kaya 10,010 zilitambuliwa kama kaya maskini sana katika vijiji vyote 94, na jumla ya kaya 9,989 zilijaziwa madodoso katika vijiji hivyo.
2:2 KUHAKIKI WALENGWA
Baada ya kaya masikini sana kubainishwa, majina yao yalipelekwa kwenye mfumo maalum TASAF Makao Makuu ambapo Mfumo huo unachuja kujua ni ipi kaya ambayo inastahili kuwa kwenye mpango na isiyostahili kwa kutumia madodoso ambayo yalijazwa kipindi cha kuzitambua kaya masikini. Majina ya kaya masikini yalirejeshwa na baadhi ya kaya zilibainika kuwa sio masikini.
Takwimu za kaya masikini zilihakikiwa ikiwa ni pamoja na kubainisha watoto wanaostahili kwenda shule na kupata huduma za afya. Pia jamii ilichagua wajumbe 14 kutoka katika kila kijiji ambao ndio wasimamizi wa mradi wa TASAF III katika ngazi za vijiji vyao.
2:3 KUFANYA MALIPO.
Shughuli ya kufanya malipo imefanyika kwa awamu kumi na moja (11) za miezi miwili miwili kama mchanganuo unavyoonyesha, fedha ilivyopokelewa kwa awamu zote kumi na moja kwa ngazi za halmashauri huku ikionesha kiasi kinachokwenda kwa walengwa, fedha ya usimamizi ngazi ya wilaya, kata na vijiji.
2.4 FEDHA ZA WALENGWA KUBAKI VIJIJINI
Kwa awamu zote kumi na moja, fedha za walengwa zilibaki kwasababu mbalimbali ikiwemo ya walengwa kuhama vijiji vyao, kufariki, walengwa kutohudhuria siku za malipo .
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa