Jumla ya Vikundi 111, vikijumuisha makundi maalumu ya Wanawake, Vijana pamoja na Watu wenye Ulemavu, vimeweza kupatiwa mikopo yenye thamani ya kiasi cha Shilingi 1,156,750,000/= Wilayani Geita, ikiwa ni juhudi za Serikali za kuhakikisha wananchi wanajikwamua kiuchumi.
Akizungumza mapema, tarehe 10,Juni kwenye hafla ya ugawaji wa mikopo hiyo makao makuu ya Halmashauri, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Geita, kupitia kamati ilopita ya Madiwani pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Ndg. Karia Magaro, kwa kuweza kuidhinisha utoaji wa mikopo hiyo kwenye kila robo ya mwaka.
Mhe. Komba amesema kuwa, bado uhitaji wa mikopo hiyo, inayotolewa na serikali pasi na kuwa na riba, ni mkubwa kwa kuwa bado wananchi wana dhamira ya kujikwamua kiuchumi, hivyo ameiagiza Halmashauri kuendelea na utaratibu wa kutenga fedha, kwajili ya kuinua maisha ya wananchi.
Aidha, Mkuu wa Wilaya amewataka wanufaika wajitahidi kuibua miradi yenye tija, ili fedha walizozipata ziweze kuwasaidia kwenye malengo yaliyokusudiwa, na mikopo hiyo iweze kurudi kwa wakati ili kusudi na wengine pia waweze kupata.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ndg. Karia Magaro amesema kuwa, suala la utoaji wa mikopo hiyo ni kubwa, hususani kwenye nyanja ya kuiingizia kodi serikali kwa kuwa inachangiia mzunguko wa fedha kuongezeka ndani ya Halmashauri, na hivyo kutoa rai kwa wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia vizuri.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa