HOTUBA YA MKURUGENZI WA HALAMSAHURI YA WILAYA YA GEITA WAKATI WA UGAWAJI MAKABATI NA BAISKELI TAREHE 23 JANUARI 2018
Mkurugezi wa Shirika la JSI Kanda ya Ziwa
Mratibu wa Muunganiko wa huduma na rufaa na wafanyakzi wote wa JSI Tanzania.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita,
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Maafisa Ustawi wa Jamii wote,
Wasimamizi wa wasimamizi wa Mashauri ya watoto,
Wafanyakazi wa halamashauri ya Wilaya ya Geita.
Waandishi wa Habari,
Mabibi na mabwana,
Habari ya Asubuhi!
Napenda Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai na nguvu anazonipatia ili niweze kuhudumia wananchi. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa shirika la JSI kupitia mradi wa uimarishaji mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii ngazi ya Jamii kwa kuwa nasi bega kwa bega katika kuwahudumia wananchi wa Geita na Tanzania kwa ujumla wake.!
Napenda kutoa pongezi kwa kitengo cha ustawi wa jamii Halmashauri wilaya ya Geita kwa utendaji uliotukuka wa kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka kuhudumia makundi yaliyo katika mazigira hatarishi hasa watoto walio katika mazingira hatarishi na jamii kwa ujumla wake.
Pia napenda kutoa shukrani kwa wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii (CCW) kwa kujitolea kuwahudumia watoto walio katika mazingira hatarishi Mungu awazidishie Baraka kwa kila mtendalo, pia napenda kuchua fursa hii kuwapongeza wasimamizi wa wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii (supervisors) kwa kazi mnayofanya japokuwa mna majukumu mengi lakini hamjasita kuweka maslahi ya watoto mbele katika kuwahudumia.
Shukurani za dhati kwa shirika la JSI kwa kushirikiana nasi kuanzisha mfumo shirikishi wa mashauri ya watoto (NICMS) kwa kutoa mafunzo kwa Walimu wa walimu, Wasimamizi wa wasimamizi wamashuri (Supervisors), maafisa ustawi wa jamii wasaidizi (PSW), Wasimamizi wa mashauri ya watoto (CCW),Ugawaji wa vitendea kazi ambavyo ni kama Baiskeli na makabati kwa ajili ya usimamizi na utunzaji kumbukumbu na taarifa za watoto.
Tumekuwa tukifanya kazi na Shirika la JSI kwa ukaribu katika shughuli mbalimbali za kupambana na kudhibiti UKIMWI na mfumo jumuishi wa mashauri ya watoto ni moja wapo ya shughuli tunazofanya kwa pamoja ili kuweza kufiki lengo la 90 90 90 ifikapo mwaka 2020.
Ninatambua kwamba mmesaidia Halmashauri ya Wilaya ya Geita vifaa vya kutolea huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi ambavyo ni baiskeli 32 na makabati 13, ni msaada muhimu kwa kuendeleza huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi na jamii kwa ujumla.
Kwa niaba ya Wananchi wa Geita na Tanzania napenda kuchukua fursa hii kushukuru kwa msaada mnaotoa katika jamii kuwafikia na kuwahudumia watoto walio katika mazingira hatarishi. Mchango wenu ni muhimu sana kwa Nchi hii na tumejidhatiti na tumejipanga kufikia malengo ya dunia ya kupambana na UKIMWI na kufikia lengo la 90-90-90 kwa maana ya asilimia 90 ya watu wote wenye maambukizi kujua hali yao, 90% ya watu wote waliogundulika kuishi na maambukizi ya VVU wamejiunga na huduma za matunzo na matibabu, 90% ya waliojiunga na huduma za tiba na matunzo wawe wamepunguza makali ya virusi mwilini.
Pia nipende kuchukua fursa hii kuomba kitengo cha Ustawi wa Jamii, idara ya afya na Maendeleo ya jamii kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa shirika la JSI-CHSSP kutekeleza majukumu yao.
Mwisho napenda kutoa shukrani kwa wale wote waliohudhuria katika zoezi hili muhimu la ugawaji vitendea kazi na imani yangu kwamba vitendea kazi hivi vitaleta tija na kuboresha mfumo jumuishi wa mashauri ya watoto(NICMS) katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita na Taifa kwa ujumla.
MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA (ALI A. KIDWAKA)
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa