Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba ameonyesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa Ofisi ya Kata, Bugulula, huku akipongeza juhudi za Halmashauri ya Wilaya ya Geita katika kusimamia ukamilishaji wa jengo hilo la Utawala linalotarajiwa kuzinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, mapema mwezi Septemba.
Mradi huo ambao mpaka sasa umefikia 83%, unatarajiwa kugharimu kiasi cha Tshs. 138,819,680/= mpaka kukamlika kwake, fedha zinazotokana na mapato ya ndani, huku pia ukijumuisha nguvu ya wananchi kwenye hatua za awali za uchimbaji wa msingi wa jengo hilo.
Akizungumza tarehe 5, Juni mbele ya wananchi waliojitokeza katika Kata ya Bugulula, akiambatana na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT) kwenye ziara yake maalumu ya ukaguzi wa Njia ya Mwenge na miradi inayotarajiwa kuzinduliwa na mwenge huo, Mhe. Komba ameitaka Halmashauri kuogeza kasi kwenye hatua za ukamilishaji wa mradi huo ili uweze kukamilika mapema, sambamba na kuhakikisha huduma zote za msingi zinapatikana kwenye mradi huo.
Mhe. Komba pia ametoa maagizo kwa Wahandisi kuhakikisha wanaongeza nguvu, pamoja na kutumia ujuzi walionao kwenye kuwaelekeza mafundi waweze kukamilisha mradi huo kwa ubora na kwa viwango stahiki.
Ziara hiyo ilijumuisha pia ukaguzi wa Mradi wa Barabara ya Km 1.1 ya lami nyepesi Kata ya Nzera, Shule ya Sekondari ya Amali, Chibingo-Nyamigota, Mradi wa Maji eneo la Inyala pamoja na Kikundi cha Vijana, Katoro.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa