Huduma za wagonjwa wa nje (OPD) na huduma za wagonjwa wa ndani au wagonjwa waliolazwa (IPD). Huduma za Wagonjwa wa ndani hutolea katika vituo vya afya.
Huduma ya afya ya mama na mtoto.
Huduma za chanjo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano (5) hutolewa katika vituo vya afya na zahanati zote.
Huduma za VVU na UKIMWI hutolewa katika vituo vya afya.
Kupambana na ugonjwa wa malaria kwa kugawa vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu.
Kushughulikia upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi.
Dirisha la Wazee pamoja na kuwapatia wazee(60+) kadi za CHF.