Wilaya ya Geita ni moja ya wilaya 5 zinazounda mkoa wa Geita. Ilipata hadhi ya kuwa wilaya mwaka 1962.Kipindi hicho iliitwa Geita province.Wilaya ya Geita ipo kati ya mita 1,100 hadi 1,300 kutoka usawa wa bahari.Pia ipo katika latitudi 208 hadi 3028 kusini mwa mstari wa ikweta na longitudi 32045 na 370 mashariki mwa mstari wa Greenwich.
Kabla ya Uhuru wa Tanzania bara (Tanganyika),wilaya ya Geita ilikuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 16,638 ambapo nchi kavu ilikuwa ni kilomita za mraba 10,123.94 na maji ilikuwa ni kilomita za mraba 6,514.06. Katika kipindi hicho Geita ilikuwa na idadi ya watu wapatao 371,407. Mnamo mwaka 1975 wilaya ya Geita iligawanywa na kupata wilaya ya Sengerema.Baada ya kugawanywa kwa wilaya hizi mbili, Wilaya ya Geita ilibaki na kilometa za mraba 7,825 ambapo nchi kavu ni kilometa za mraba 6,775 na maji ni kilometa za mraba 1,050.
Mnamo mwaka 2013 wilaya ya Geita iligawanywa tena na kupata wilaya ya Nyang'hwale.Wilaya ya Geita ina Halmashauri mbili ambazo ni "Halmashauri ya wilaya ya Geita na Halmashauri ya Mji".Halmashuri ya Geita ina ukubwa wa kilomita za mraba 5,366.7(4,316 nchi kavu na 1,050 maji).
Asili ya jina Geita: Neno Geita limetokana na maneno matatu ya kabila la Wayango (Warongo) ambayo ni Akabanga keita abhantu likiwa na maana kupotea kwa mazingara ambayo yalikuwa kwenye mlima huo wa Akabanga keita abhantu uliokuwa ukitumiwa na warongo kama eneo la mitambiko ya jadi.Jina hili la Geita lilikuwa maarufu kutokana na wazungu kushindwa kutamka maneno Akabanga keita abhantu na hivyo kukatisha kuwa Geita hadi leo.Makabila yaliyokuwepo ya Wazinza, Wasukuma,Wasumbwa na Wasubi wakaigiza matamushi ya wazungu Geita na hivyo neno la Akabanga keita abhantu likaanza kupotea polepole hadi leo.
Wilaya ya Geita hupata mvua yenye wastani wa 900mm-1000mm katika tarafa za Busanda na Kasamwa,pia hupata mvua za wastani wa 1000mm-1300mm katika tarafa za Butundwe na Bugando.
shughuli za uchumi kaika wilaya ya Geita ni;kilimo,ufugaji,uvuvi na uchimbaji wa madini ya dhahabu.
UTAWALA KABLA YA WAKOLONI
Kabla ya kuingia kwa wakoloni (Wajerumani na Waingereza) Geita ilikuwa na tawala za asili saba (7) ambazo ni:
UTAWALA
|
CHIFU/MTEMI
|
MAKAO MAKUU
|
Busambilo
|
Ludomya Ng’hwele
|
Nyarubele
|
Msalala
|
Musa Chasama Mbiti
|
Kitongo
|
Buyombe
|
Mgunga Kadama
|
Busanda
|
Buchosa
|
Paulo Lukakaza
|
Nyakalilo
|
Kharumo
|
Alexander Gerevas
|
Kharumo
|
Bukoli
|
Mganila Nonga
|
Bukoli
|
Mwingiro
|
Nyorobi Mapumba
|
Idetemya Mwingiro
|
Wakoloni wa kwanza kuingia Geita walikuwa ni wajerumani ambao utawala wao ulikuwa ni wa moja kwa moja(Direct rule) na hivyo kushindwa kabisa kwani wawakilishi wao waliokuwa wakiletwa toka makao makuu Bagamoyo(Pwani) walikuwa wakiuwawa na wenyeji.
Utawala wa pili ulikuwa wa waingereza baada ya vita kuu ya pili ya dunia,ambao wao walitumia utawala usikuwa wa moja kwa moja(Indirect rule) yaani kwa kuwatumia machifu/watemi wa maeneo husika ili kutekeleza azma/malengo yao.
Eneo la mji wa Geita aliwekwa Liwali Petro Nyango ambaye alifanya kazi chini ya utawala wa kwa eneo la mjini.
BARAZA LA JADI (NATIVE AUTHORITY)
Baraza hili lilikuwa chini ya uangalizi wa Mkuu wa Wilaya(DC) wa kikoloni,liliundwa na watemi 7 na liwali 1.Mwenyekiti wa baraza hilo alitokana na watemi hao.Aidha katibu wa baraza hilo alitokana na watemi au karani kutoka ofisi ya DC.
Makao makuu ya baraza hilo yalikuwa mjini Geita eneo jirani na Benki ya CRDB, kila mtemi alijengewa nyumba ya kupumnzikia na kulala.
MAJUKUMU YA BARAZA HILO
Historia ya Wahe. Wenyeviti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita
Na
|
Jina kamili
|
Mwaka alioanza
|
Mwaka alioonddoka
|
1.
|
Samwel S. Mabeyo
|
1984
|
1988
|
2.
|
Edward K. Sumuni
|
1988
|
1997
|
3.
|
Said S. Mahuma
|
1997
|
2000
|
4.
|
Jeremia M. Ikangala
|
2000
|
2010
|
5.
|
Musukuma J. Kasheku
|
2010
|
2011
|
6.
|
Elisha H. Lupuga
|
2011
|
-
|
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa