MAJUKUMU YA KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI NA UTEKELEZAJI WAKE
Mkuu wa Kitengo
Wankyo Marwa
Kwa mujibu wa kifungu cha 48(1) cha sheria ya fedha za Serikali za Mitaa namb.9 ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa mwaka 2000, na kama ilivyonukuliwa katika Amri ya 13(1) ya Kanuni za Fedha katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa ya mwaka 2009 kinabainisha kuwa “Hesabu za kila Halmashauri ya Wilaya na za Mamlaka za Miji zitakaguliwa na Mkaguzi wa Ndani aliyeajiriwa na mamlaka husika” mwisho wa kunukuu. Ukaguzi wa Ndani unafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ya fedha kama inavyotolewa na serikali mara kwa mara. Ukaguzi wa Ndani pia unazingatia Viwango vya Kimataifa vya Ukaguzi wa Ndani(International Standards for the Professional Practice of Internal Auditing (Standards) vinavyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya ukaguzi wa ndani(The Insitute of Internal Auditors) ambavyo vimeridhiwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) Tanzania.
2.0 Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
Kwa mujibu wa AMRI ya 14(4) ya Memoranda ya fedha katika Serikali za Mitaa ya mwaka 2009 na makubaliano ya majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kati ya Uongozi wa Halmashauri na Mkaguzi wa Ndani (Charter for Internal Audit Services), majukumu ya Mkaguzi wa ndani ni pamoja na;
(ii) Kufanya tathmini ya kazi mahsusi na mifumo kama ifuatavyo:
Kupitia na kutoa taarifa juu ya mapato na matumizi ya fedha za umma kama yanazingatia Sheria, Kanuni,Taratibu na Mikataba iliyopo. (Financial Audits)
Kuhakiki na kutoa taarifa juu ya shughuli za utekelezaji wa miradi ya maaendeleo na kubaini kama thamani ya fedha zilizotumika zimepatikana (Performance Audits or Value for Money Audit).
Kufanya ukaguzi wa Rasrimali watu (Human Resource Audits).
Ukaguzi wa manunuzi ya umma (Procurement Audits).
Kutoa ushauri wa namna ya kuongeza thamani katika masuala mbalimbali kwa makubaliano na mteja (Consulting Activities).
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa