Halmashauri ya wilaya ya Geita ina joto ridi linaloanzia 17oC mpaka 30oC na ina wastani wa kiasi cha mvua cha ujazo wa 1200mm kwa mwaka ampapo mvua huanza mwezi Oktoba mpaka Januari na mwezi Machi mpaka Julai. Pia unyevunyevu wa hewa upo kati ya 35% mpaka 60%.
Halmashauri ya wilaya Geita ina eneo linalofaa kwa kilimo hekta 327,000. Eneo linalotumika kwa kilimo ni hekta 146,414. Aina ya udongo unaopatikana ni tifutifu(tarafa za Bugando,Butundwe na Kasamwa),kichanga(tarafa ya Kasamwa) na nduha/kaollimite(tarafa za Bugando,Butundwe na Kasamwa).
Eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni Hekta 13,160. Kilimo cha Umwagiliaji kinafanyika kwa mazao mbalimbali kama vile Mpunga, Mbogamboga, Matunda, Mahindi na Maharage ya mabondeni. Mazao ya biashara yaliyoshamiri ni mpunga na nanasi(kata za Bugulula,Nzera na Kakubilo). Aidha mazao mengine ya biashara yanayohitaji uwekezaji kwa sasa ili kuendana na sera ya Tanzania ya viwanda ni miwa,muhogo na alizeti.
Eneo linalolimwa kwa umwagiliaji ni Ha. 8,009, vyanzo vya maji ni ziwa Victoria, mito isiyokauka,chemchemi na maji ya mvua. Uboreshaji wa miundombinu wa maeneo yanayofaa kwa kilimo utasaidia kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji na uzalishaji wa mazao kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa