Katika kutekeleza mpango wa huduma ya afya kwa wananchi, Halmashauri ya Wilaya Geita imeazimia kufika lengo la kuwa na vituo vya kutolea hududuma ya afya kwa kila kijiji na kata.
Katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita waliozuru katika kata tatu(3) za Nyakamwaga,Bukoli na Nyarugusu na vijiji vyake kando na changamoto kadhaa zilizobainika huduma ya afya imetajwa kuimarika hasa katika mpango wa ujenzi wa zahanati kwa kila kijiji na vituo vya afya kila kata.
Ziara ya Mkuu huyo kwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ameshiriki katika ujenzi wa zahati mbili ambazo ni zahanati ya kijiji cha Bugalahinga kata ya Nyakamwaga, zahanati ya kijiji cha ikina kata ya Bukoli na kituo cha afya cha Nyarugusu.
Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe. Diwani Elisha Halaka Lupuga ameahidi kutoa msaada wa Milioni Tano(5,000,000) kwa kila zahanati inayojengwa ili kusaidia kukamilika kwa zoezi hilo huku viongozi aliombatana nao wakiongeza nguvu kwa michango ya mifuko ya theruji na tofali.
Aidha Injiania Robert mbali na kutoa pongezi kwa Halmashauri kwa juhudi ya kufanya vijiji zaidi ya 145 kuwa na uhakika wa huduma ya afya lakini ameshauri kuwepo mapitio mapya ya baadhi ya miradi ya afya kutokana na kuonekana kuwa na matumizi makubwa ya fedha katika ujenzi wake inayokwenda kinyume na maelekezo ya matumizi ya Serikali.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa