Mafunzo yaliyodumu kwa siku mbili mfululizo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kwenye vituo vya kupigia kura, Oktoba 27 yamefikia tamati katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, huku washiriki wakitakiwa kuzingatia suala la ufanisi pamoja na uadilifu.
Akizungumza wakati akihitimisha mafuzo hayo katika Kata ya Nzera, yaliyojumuisha pia Kata za jirani zikiwemo Kata ya Izumacheli, Nkome, Nyamboge, Katoma, Lwezera na Kakubilo, Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi ngazi ya Halmashauri Bi. Sarah Yohana, amewapongeza wasimamizi hao huku akiwataka wazingatie suala la uweledi.
“Niwapongeze kwa kumaliza mafunzo lakini pia ninaamini kwamba kwa kuwa mmeaminiwa na Tume Huru ya Uchaguzi kuifanya kazi hii, mtaifanya kwa ufanisi wa hali ya juu. Tunaamini kuwa hamtatuangusha na mtaifanya kazi hii vizuri.” Amesema Bi. Sarah.
Awali wakati akiendesha mafunzo hayo, Ndg. Festo Gaudence Nsalamba amewasisitiza Wasimamizi hao kuvitambua vituo walivyopangiwa huku pia akiwataka wahakikishe wanazingatia muda kwenye vituo vyao ili kutowaingiza wapiga kura kwenye changamoto ya kutoweza kupiga kura.
Kwa upande wake, mmoja wa wasimamizi hao, Ndg. Anord Rwegoshora amesema kuwa watahakikisha wanasimamia yale waliyojifunza kwenye mafunzo hayo likiwemo suala la kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa watu wenye mahitaji maalumu ili wasiweze kupata adha kwenye zoezi la kupiga kura.
Jumla ya vituo 1288 vinatarajiwa kutumika kwenye Uchaguzi Mkuu katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita yenye majimbo matatu ya uchaguzi ambayo ni Jimbo la Geita, Katoro na Busanda.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa