Hayawi hayawii sasa yamekuwa. Leo Oktoba 29,2025 ni Siku ambayo Watanzania wameisubiri kwa hamu ili kutimiza Takwa la Kikatiba.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Alphonce Bagambabyaki ameshiriki zoezi la kupiga kura mapema leo Oktoba 29,2025.
Dkt Bagambabyaki amepiga kura katika Kata ya Nzera yalipo makao Makuu ya Halmashauri kuchagua Rais, Mbunge na Diwani.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina majimbo matatu ya Uchaguzi ambayo ni Geita, Busanda na Katoro.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa