Viongozi wa Dini Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Oktoba 20 ,2025 wamefanya Dua na Sala kuliombea Taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29.
Duah na Sala zimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ulipo Nzera ambapo Watumishi wa umma wameungana na viongozi hao kuliombea Taifa.
Pamoja na Duah na Sala , Viongozi hao wamewataka Watumishi wa umma kupendana, kushikamana na kufanya kazi kwa uadilifu kwa Maslahi ya Taifa.
Vilevile Viongozi hao wametoa wito kwa Watumishi wa umma kuwa mawakala wa amani kuelekea Uchaguzi Mkuu ili Uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa