Ujumbe kutoka Menejimenti ya Benki ya NMB, tawi la Geita, Oktoba 20, 2025 umepata nafasi ya kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ambapo Benki hiyo imemwaga udhamini wa vifaa vya michezo kwa timu za wanaume na wanawake, ikiwa ni muendelezo wa kuhakikisha timu hizo zinafanya vyema kwenye mashindano tofauti tofauti.
Akizungumza wakati wa ugeni huo, Meneja wa tawi hilo, Ndg. Daniel Rauya amesema dhima kuu ya kutoa udhamini huo ni kuchochea ari ya wanamichezo kwenye Halmashauri hiyo kushiriki katika michezo.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Alphonce Bagambabyaki ameushukuru Uongozi wa Benki hiyo kwa kuendelea kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwenye suala zima la kuhamasisha watumishi kushiriki katika michezo ili kujiweka sawa sawa kimwili pamoja na kiakili.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Halmashauri, Ndg. Elias Kachwele amesema udhamini huo ni muhimu kwa kuwa utaongeza ufanisi kwenye sekta ya michezo miongoni mwa watumishi hao.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa