Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Ndugu, Mzee Mkongea Ali kutoka Mjini Magharibi, amefungua Miradi 5 na kuweka jiwe la msingi katikia miradi 2 kati ya miradi 8 iliyokuwa katika mpango wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita iliyogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 5.4
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 zikiwa na ujumbe unaozingatia hoja, vipaumbele na mikakati ya Serikali ya awamu ya Tano ya Kuboresha Sekta ya Maji kwa kuzingatia dhana ya ushirikishwaji wa wananchi katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji umetembelea Kisima cha maji njia panda ya Iyala uliogharimu kiasi cha shilingi 22,251,000.
Pia Miradi iliyopitiwa na mbio za mwenge wa uhuru 2019 ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita ni pamoja na Ujenzi wa Madarasa 12 ya Sekondari 1 ya Katoro uliogaharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni 119 katika utekelezaji wake.
Miradi mingine ni pamoja na kuwekwa jiwe la msingi Kituo cha Afya Kakubilo kilichogharimu kiasi cha Shilingi 93,507,000, Mradi unaotekezwa na nguvu za Wananchi, Halmashauri ya Wilaya,Wahisani na Serikali kuu. Katika kilimo, Mbio za mwenge wa Uhuru 2019 ndani ya Halmashauri ya Wilaya zimepitia na kuzindua mradi ya Kitalu Shamba Salagulwa na kutembelea shamba la Nanasi Kagu, kwa lengo la kuongeza kasi ya kilimo cha kisasa na chenye tija.
Mwenge wa Uhuru 2019 Katika kuihamasisha jamii ya watanzania kuhusu Mapambano dhidi ya Rushwa, mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na mapambano dhidi ya Malaria, Mwenge umezindua klabu ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya na klabu ya kuzuia na kupambana na Rushwa katika Shule ya Sekondari Chigunga.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita tumeadhimia kusimamia kwa uadilifu miradi yote iliyokatika utekelezaji ili kuongeza hamasa kwa wananchi juu ya maendeleo katika sekta zote ili kwenda sawa na malengo ya Dira ya Taifa ya maendeleo 2025.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa