Wauguzi katika vituo vya Afya na Zahanati Pamoja na Maafisa Lisha leo Septemba 23,2025 wamepatiwa mafunzo ya Afua za Lishe ili kuwajengea uwezo katika maeneo ya kazi.
Awali akifungua mafunzo hayo katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ulipo Nzera, Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Dkt Modest Buchard amewapongeza Maafisa Lishe na wauguzi hao kwa namna ambavyo wanaendelea kutekeleza majukumu yao katika maeneo yao ya kazi.
“Niwapongeze kwa namna ambavyo mnapambana kwenye vituo vyenu vya kazi. Kama tunavyoishi nyumbani basi na maeneo ya kazi tuyapende na kuyachukulia kama sehemu yetu ya Maisha ya kila siku kwani kazini ni sehemu tunayokaa kwa muda mrefu” Amesema Dkt Modest Buchard.
Aidha Dkt Modest amewataka Maafisa Lishe na Wauguzi hao kuepuka Migogoro sehemu za kazi na kupafanya kazini kuwa sehemu salama huku akiwataka kuendelea kushikamana,kushirikiana na kuvumiliana katika maeneo ya kazi ili maisha ya kazi yaweze kwenda vizuri
Vilevile Dkt Modest katika mafunzo hayo amewaasa Waganga Wafawidhi kuvisimamia vituo vyao vya kazi kwa weledi ikiwa ni Pamoja na kuwahimiza watumishi kuvaa sare wakati wote wa muda wa kazi ili kuwa nadhifu.
Kwa upande wake Afisa Lishe Bi Ummy Kileo amewataka Maafisa Lishe kulipa uzito swala la Lishe katika maeneo ya kazi wanapotoa huduma ikiwa ni Pamoja na Kutengeneza ratiba ya afya na lishe na kuzitekeleza Pamoja na kuweka kumbukumbu kwa kazi ambazo zinafanyika ili ziweze kufanyiwa kazi katika ngazi nyingine
Pamoja na hayo Bi Ummy ameeleza Mikakati ya kuboresha vituo vya kutolea huduma ili kuendelea kulipa uzito swala la lishe kwa kuendelea Kuimarisha huduma ya mama baba na mtoto kwa kutoa elimu ya lishe, Upatikanaji wa bidhaa za lishe katika meneo ya kutolea huduma,Kufanya tathmini ya lishe na kutunza kumbukumbu ili kupata takwimu sahihi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa