Timu ya Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Geita , Oktoba 09,2025 imefanya kikao na timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita chenye lengo la kutatua changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya Ukamilishaji wa Miradi ya fedha za BOOST (Bakaa) yenye Jumla ya Shilingi Bilioni 3.2.
Katika Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji-Nzera kimejadili changamoto zinazotokana na Mafundi ujenzi, wazabuni pamoja na usimamizi wa miradi hiyo ili iweze kukamilika na kutoa huduma kwa jamii.
Pamoja na utekelezaji wa Miradi ya Bakaa, Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2025/26 ambapo fedha kutoka Serikali kuu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.3 huku mapato ya ndani ikiwa ni Shilingi Bilioni 6.1.
Timu ya Wataalam Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita (CMT) wakiwa katika Kikao katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kujadili utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa