GEITA
Wakuu wa idara na vitengo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita wamefanya ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea kujengwa ambapo wakuu wa idara wametembelea shule ya Nyamigota, Ludete, Mji mwema, Bahari, Simbachawene, Magenge, Machinjio ya Ludete na Soko la dhahabu katika Mamlaka ya mji mdogo wa Katoro.
Ziara hiyo ya kikazi imefanyika Oktoba 16, 2025 ambapo wakuu wa idara wamekagua na kuhakiki miradi yote ambayo inaendelea kujengwa na mingine kumaliziwa kutokana na fedha za serikali kuu, mapato ya ndani na BOOST ambapo baadhi ya miradi imefikia katika hatua nzuri ya ujenzi.
Timu ya Menejimenti (CMT) ikiwa kwenye baadhi ya miradi inayoendelea kutekelezwa kupitia fedha za mapato ya ndani, serikali kuu na wafadhili
Kwa upande wa miradi ambayo inaendelea kujengwa , wasimamizi wake wametakiwa kuhakikisha wazubuni wanaochukua tenda wanapeleka vifaa vyote vya ujenzi kwenye maeneo husika ya miradi hiyo ili kuepuka kadhia ambazo zitafanya kucheleweshwa kumalizika kwa miradi hiyo kwa wakati.
"sehemu ambayo kuna changamoto ya wazabuni wa awali ambao wameshindwa kuleta vifaa vya ujenzi kwa wakati wavunjiwe tenda zao ili watafute wazabuni wengine ambao wataleta vifaa kwa wakati ili kukamilisha miradi kwa muda uliopangwa." Amesema Mhandisi Shilingo.
Aidha, baada ya kutembelea miradi hiyo ya maendeleo , wakuu wa idara wametoa tathmini zao kwa wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha kuwa wanawasiliana na wazabuni wote wanaopeleka vifaa (materials) vya ujenzi ili kuharakisha zoezi la ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo kwani majengo hayo yanahitajika yaanze kutumika na wanafunzi.
Mafundi ujenzi wakiendelea na kazi kukamilisha miradi
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa