Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita Mhe Grace Kingalame Septemba 24, 2025 ametembelea Banda la Maonesho la Halmashauri ya Wilaya ya Geita katika viwanja vya Dkt Samia Manispaa ya Geita.
Akiwa katika banda hilo Mhe Grace amevipongeza vikundi vya Wajasiriamali kwa namna ambavyo vinajibiidisha baada ya kupokea Mikopo ya Asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kupitia Mapato ya ndani.
Kwa Upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Jonas Kilave amemueleza Mkuu huyo wa Wilaya bidhaa zinazopatikana ndani ya banda hilo zikiwepo Asali, mafuta ya kupika, dagaa, mbegu za mazao nk.
Mhe Kingalame ameipongeza Halmashauri kwa kuendelea kuvisimamia vikundi vya Wajasiriamali huku akiwakumbusha Kujitokeza kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.
Maoenesho hayo yamebebwa na Kauli mbiu isemayo: "Ukuaji wa Sekta ya Madini ni Matokeo ya Matumizi ya Teknolojia Sahihi na Uongozi Bora, Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa