Timu ya Uhamasishaji na matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA) Wilaya ya Geita leo jumatatu Septemba 27, imeanza rasmi kutoa Semina kwa wadau mbalimbali kuhusu matumizi ya TEHAMA Katika shughuli za uzalishaji mali.
Semina hiyo imetolewa katika ukumbi wa Gedeco Mjini Geita ikiwa ni moja ya majukumu yanayotakiwa kufanyika katika Maadhimisho ya wiki ya TEHAMA ki Wilaya iliyoanza leo hadi Oktoba mosi mwaka huu.
Wajumbe wakiwa Vyama vya Amicos,viongozi wa wafanyabiashara,na viongozi wa vyama vya ushirika wamepatiwa Elimu ya namna TEHAMA inavyoweza kuwasaidia katika shughuli za kiuchumi kwa kutangaza biashara zao,kutambua fursa za kibiashara,kutambua huduma zitolewazo na Serikali na hata kutambua na kutumia huduma mtandao.
Msajigwa Alfred Kasambo Mwezeshaji ambaye pia ni Mkurugezi wa Kampuni binafsi ya Infodigtech for Community Empowerment akiwawezesha wajumbe amesema kuwa, ‘‘ TEHAMA ni biashara hivyo ni vyema kuchangamkia fursa hiyo kwa kujifunza na kuitumia kwa faida ili kufahamu mambo mbalimbali ya msingi kama vile tenda za Serikali na Kampuni binafsi, mpango wa uuzaji bidhaa nje, masoko na bei za bidhaa.
Awali akitoa utangulizi katika Semina hiyo Bw.Frank Makonda mwezeshaji ambaye pia ni Afisa TEHAMA Halmashauri ya Wilaya ya Geita amesema kuwa TEHAMA imeleta mapinduzi makubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwemo uhuru wa kujieleza.
Ameendelea kusema licha ya kuwa na faida kubwa kwa wananchi kumekuwepo na changamoto ambazo zimeambatana na mafanikio hayo kama vile uhalifu wa kwenye mitandao, chanzo cha maadili mabaya katika jamii, na nyingine nyingi.
Makonda amesema kuwa kwa kulitambua hilo Serikali kupitia mbio maalumu za mwenge mwaka huu 2021 imeamua kuja na kauli mbiu ya ‘’TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu itumie kwa usahihi na uwajibikaji’’ suala linalowataka wadau wote wa TEHAMA zikiwemo taasisi zilizopewa dhamana hiyo kutoa elimu kwa jamii juu ya matumizi sahihi kwa maendeleo ya nchi yetu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa