Nzera-Geita
Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita umefanyika leo Desemba 04,2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Akifungua Mkutano huo Katibu Tawala Wilaya ya Geita Bi Lucy Beda amewasihi Madiwani hao kwenda kuwatumikia wananchi ili matarajio yao yaweze kutimia.

Katibu Tawala Wilaya ya Geita Bi Lucy Beda akizungumza katika Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo amewataka Waheshimiwa Madiwani kuwatumikia Wananchi walio wachagua ili kutimiza matarajio yao
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Alphonce Bagambabyaki akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa kipindi ambacho Baraza lilivunjwa, amewapongeza Waheshimiwa Madiwani kwa Kuchaguliwa na kuaminiwa na wananchi kutekeleza shughuli za maendeleo ndani ya Halmashauri ,
" Ni imani yetu mtashirikiana kwa umoja, hekima na uwazi katika kupanga, Kushauri na kutekeleza mipango ya maendeleo itakayoboresha maisha ya wananchi katika nyanja zote ikiwepo elimu, afya, miundombinu, uchumi na huduma za kijamii" Amesema Dkt Bagambabyaki.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashaur ya Wilaya ya Geita Dkt Alphonce Bagambabyaki akizungumza Katika Kikao cha Kwanza cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita na kuwataka Waheshimiwa Madiwani kwenda kutekeleza mipango ya maendeleo itakayoboresha maisha ya wananchi katika Halmashauri
Pamoja na shughuli nyingine katika Mkutano huo Waheshimiwa Madiwani wamekula kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Geita Mhe Faraja Thomas pamoja na ahadi ya uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya Kamishina wa Maadili Bw Kweka.

Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Jumanne Sengo Misungwi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ludete akizungumza na Waheshimiwa Madiwani katika Kikao cha Kwanza cha Baraza la Madiwani.Mhe Misungwi amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kupata Kura 50 kati ya 51 za Wajumnbe wote waliompigia kura ya ndio
Aidha katika Mkutano huo Mhe Jumanne Sengo Misungwi Diwani wa Kata ya Ludete amechaguliwa kwa Kura za Ndio 5o kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo kura 1 ilisema Hapana huku Diwani wa Kata ya Nkome Mhe Sylvester Christopher Kahesi akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kura 51 akishindana na Diwani wa Kata ya Butundwe Mhe Charles Luzukana wa chama cha ACT Wazalendo aliyejitoa katika kura za ndio na hapana akimuunga mkono Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.

Mhe Sylvester Christopher Kahesi Diwani wa Kata ya Nkome akiwashukuru Waheshimiwa Madiwani mara baada ya kuchaguliwa kwa kura zote za ndio Katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Mkutano huo ni wa kwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025 ambapo Halmashauri Halmashauri ya Wilaya ya Geita ilishiriki Uchaguzi huo kwa majimbo matatu ya Uchaguzi ambayo ni Geita, Busanda na jimbo jipya la Katoro.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa