Nzera-Geita
Wizara ya Kilimo imetoa zana za Kilimo ambazo ni Matrekta 5 na Pawatila 16 pamoja na viambata vyake.
Akipokea hati ya makabidhiano ya vifaa hivyo kutoka kwa Afisa Manunuzi Wizara ya Kilimo Ndg Stephen Ikanga, Desemba Mosi, 2025 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Alphonce Bagambabyaki ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kutoa zana hizo kuwasaidia wakulima katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
" Tunashukuru Serikali inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia zana hizi kwani Uhitaji ni mkubwa sana kwani shughuli za Kilimo hususani zao la Mpunga zinafanyika kwa kiasi kikubwa katika maeneo yetu" Amesema Dkt Alphonce.
Vile Vile Dkt Alphonce amesema zana hizo zitawasaidia wakulima wakubwa na wadogo na kwa kuzingatia jiografia ya Maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita Pawatila zitatumika kwa maeneo ambayo Trekta hazitaweza kufika na kwa wakulima ambao hulima ekari chache.
Pamoja na hayo Kaimu Mkurugenzi amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Geita Mhe Joseph Kasheku Musukuma kwa juhudi zake katika upatikanaji wa zana hizo ambazo zitaenda kuongeza uzalishaji ndani ya Halmashauri na kukuza uchumi wa wananchi.
Lengo la kutoa zana hizo ni kuanzishwa kwa kituo cha Zana za Kilimo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo wakulima wataweza kukodi zana hizo kwa gharama ndogo ili kufanikisha shughuli za kilimo katika maeneo yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa