Waziri wa wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi Maalum Dk. Dorothy Gwajima ameonesha kufurahishwa na huduma zinazotolewa na benki ya biashara Tanzania Tcb kwa kuwa zinalenga pia makundi maalum.
Waziri Gwajima ameeleza hayo baada ya kutembelea banda la benki hiyo katika tamasha la maendeleo Tanzania lililofanyika uwanja wa Ccm Kalangalala Mjini Geita.
Waziri Gwajima akieleza kufurahishwa na huduma za benki hiyo ya Tcb ameeleza kuwa benki hiyo imekuwa rafiki kwa serikali ambapo pia inatoa huduma kwa makundi maalum.
Meneja wa Idara ya mikopo wa benki hiyo ya Tcb makao makuu Dar es Salaam Emmanuel Nyange ameeleza kuwa benki hiyo imeasisi huduma za makundi maalumu tangu miaka 10 iliyopita.
Wakati huohuo Waziri Dk. Dorothy Gwajima wakati akifunga tamasha hilo la Maendeleo Tanzania ameeleza kuwa vitendo vya ukatili kwa wanawake vimekuwa vikimega asilimia mbili ya uchumi wa dunia kwa ajili ya kuhudumia wahanga wa matukio ya kikatili badala ya kufanya shughuli za maendeleo.
Waziri Gwajima pia ameeleza kuwa kwa mujibu wa ripoti ya benki ya dunia inaonesha kuwa baadhi ya nchi duniani zinatumia hadi asilimia 3.5 ya pato la ndani kushughulikia vitendo vya ukatili wa kijinsia Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ameeleza kuwa lengo la tamasha hilo la Maendeleo ilikuwa ni kuonesha fursa na kutoa elimu mbalimbali.
Tamasha hilo lilianza novemba 25 na limefungwa novemba 30 mwaka huu huku likienda kwa kaulimbiu isemayo “Zijue fursa,Imarisha uchumi,kataa ukatili, Kazi iendelee.”
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa