WAZIRI wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye (MB) Julai 17 amefanya ziara Mkoani Geita katika Kata ya Nyamigota kijiji cha Luhuha Jimbo la Busanda Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo amekagua Mnara wa simu uliojengwa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ulionzishwa na serikali ili kuwezesha huduma za mawasiliano vijijini.
Mhe Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye(MB) akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Geita na Wananchi Kata ya Nyamigota kijiji cha Luhuha Jimbo la Busanda Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Mhe Nape amesema misingi ya Wizara ni kuwezesha upatikanaji wa huduma ili kila Mtanzania apate huduma popote, huduma zipatikane kwa ubora na ziweze kupatikana kwa urahisi kwa watumiaji huku zikiwa salama na kuweza kuleta matokeo mazuri.
Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye(MB) ameeleza kuwa Mradi wa ujenzi wa Minara 758 ya simu kwa Teknolojia ya 2G, 3G na 4G utawanufaisha Watanzania Milioni 8.5 waishio katika maeneo ya vijijini
Aidha Mhe Waziri Nape (MB) amewataka wananchi wa Kata hiyo kuhakikisha wanatumia Teknolojia ya Mawasiliano kama fursa katika kufanya biashara kupitia huduma zinazotokana na mawasiliano na si kutumia Teknolojia vibaya kwani Teknolojia huacha alama.
Pamoja na hayo Mhe Waziri Nape (MB) amesema Serikali imeleta kiasi cha Fedha shilingi Bilioni 2.2 kwa ajili ya kutatua changamoto ya Mawasiliano ndani ya mkoa wa Geita katika ujenzi wa miundombinu ya huduma za mawasiliano vijijini.
Bi Justina Mashiba Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) amesema zaidi ya wananchi laki 2 wa wa Mkoa wa Geita watanufaika na Minara 17 ya Mawasiliano ya simu inayojengwa katika Mkoa wa Geita katika kata 16 na vijiji 27 ambapo Serikali imetoa ruzuku ya Shilingi Bilioni 2.2
Mh.Nauye amesema matarajio ya Serikali ni kujenga jumla ya minara 758 kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Kwa mradi wa Miundombinu ambayo inajengwa Tanzania bara katika mikoa 26 huku akisema Serikali inatoa ruzuku zaidi ya Bilioni 266 ya ujenzi wa Minara hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuupatia Mkoa wa Geita Shilingi Bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa Minara ya Mawasiliano maeneo ya vijijini.
Geita ni mkoa wa 10 kwa kuwa na idadi kubwa ya laini za simu ambapo hadi mwezi Machi 2024 jumla ya laini 2,417,513 zilikuwa zimesajiliwa kutoka laini 2,050,124 mwezi Juni 2022.
Jumla ya Minara 55 imejengwa mkoani Geita kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika wilaya 5 za Mkoa wa Geita ambazo ni Bukombe (10) Chato (9) Geita Dc (10) Mbogwe (18) na Wilaya ya Nyang’wale (8) ambapo wananchi 643,354 wananufaika kupitia minara hiyo na katika Minara 758 Tanzania Bara jumla ya minara 17 inatarajiwa kujengwa Mkoani Geita katika kata 16 za Wilaya za Bukombe, Chato, Geita na Mbogwe na kunufaisha wakazi 241,240.
Mhe Nape Nnauye(MB) akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Geita Mji Mhe Kanyasu na Wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya na Mji Mkoani Geita alipofanya Ziara ya Kukagua hali ya usikivu wa simu na redio mkoani geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa