Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameendelea kuwatoa hofu wakulima wa pamba mkoani Geita na Tanzania kwa ujumla kuwa pamba yao yote itanunuliwa msimu huu.
Waziri Mkuu ametoa hakikisho hilo katika ziara yake ya maeneo mbalimbali ya wakulima wa pamba mkoani Geita ambapo amesema ununuzi wa pamba umekuwa wa kusuasua kutokana na hali ya soko la dunia kuwa tete
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezidi kusisitiza kuwa bei ya kilo moja ya pamba ni shilingi 1,200 na kuwataka wakulima wa zao hilo wasikubali kuuza pamba yao chini ya bei hiyo.
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa ili waweze kuwachagua viongozi waadilifu na wanaoweza kuwatetea wapiga kura wao.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa unatarajia kufanyika nchi nzima hapo Novemba 24 mwaka huu
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa