Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Hadija Said, Januari 20 ameongoza wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi Halmashauri ya Wilaya ya Geita kukagua miradi ya Maendeleo jimbo la Geita.
Mhe Hadija ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyamigota ametoa pongezi kwa Watumishi wa Halmashauri kwa namna ambavyo wanasimamia miradi inayotekelezwa na Serikali.
Pamoja na pongezi hizo Makamu Mwenyekiti huyo amewataka mafundi wanaotekeleza miradi hiyo kuweka bidii ili miradi ikamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma.
" Jitihada ziongezeke na iwapo kuna mkwamo wowote basi mtoe taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji ili hatua za haraka zichukuliwe" amesisitiza Mhe Hadija katika ziara hiyo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Lwezera Mhe Chinchina amewataka wahandisi kuzingatia kuweka mifumo ya kuvuna maji kwenye shule ili yaweze kusaidia katika matumizi mbalimbali.
" Tunapokuwa na Mifumo ya kuvuna maji itasaidia uwepo wa maji ya kutosha na kusaidia kuzuia magonjwa ya milipuko" Amesema Mhe Chinchina.
Aidha wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi wamempongeza Diwani wa Kata ya Kakubilo Mhe Kessy kwa kutoa eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Ikigijo.
Vilevile Kamati hiyo imewaagiza mafundi kuongeza nguvu kazi ya kutosha ili kuweza Kukamilisha miradi ndani ya muda kwa ubora unaotakiwa.
Pamoja na kuwasisitiza mafundi ujenzi kuongeza nguvu kazi, Kamati hiyo imetoa wito kwa Watumishi wanaosimamia wazabuni wanaomba kazi za miradi kupitia mfumo wa Nest kuepuka kuwapa kazi wazabuni wanaochukua kazi nyingi ilihali hawana uwezo wa kuzitekeleza kwa wakati na kusababisha kuchelewa kukamilika kwa miradi
Kamati ya Fedha na Uongozi ikiwa katika Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi Shule ya Sekondari Nyakaduha. Mradi huu una Thamani ya Shilingi Milioni 100,000,000 kutoka Serikali Kuu.
Kamati ya Fedha na Uongozi ikiwa katika Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Amali Nzera wenye thamani ya Shilingi Milioni 584,280,029
Kamati ya Fedha na Uongozi ikiwa katika Mradi wa Ukamilishaji wa Bweni Shule ya Sekondari Kakubilo wenye thamani ya Shilingi Milioni 60,000,000 kutoka Serikali Kuu. Kamati hiyo imewataka wanafunzi wanaotumia Bweni hilo kulitunza
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa