Wananchi wa Kata ya Katoro, mapema leo Septemba 20, 2025 wamejitokeza kuadhimisha siku ya Usafishaji Duniani ikiwa ni mwendelezo wa juhudi za kupambana na changamoto ya udhibiti wa taka duni katika jamii.
Kampeni hiyo iliyahusisha maeneo yenye idadi kubwa ya watu yakiwemo Masoko, Vituo vya Abiria, Migahawa, Vituo vya Afya, pamoja na usafi binafsi kwenye maeneo ya makaazi ambapo wananchi waliweza kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika zoezi hilo lililoanza majira ya asubuhi.
Aidha, siku hii pia iliadhimishwa kwa Wataalamu wa Afya kutoka Kitengo Cha Udhibiti Taka na Usafi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, kutoa elimu kwa wafanyabiashara pamoja na wakaazi wa eneo hilo juu ya namna bora ya kuhifadhi taka ili kuwa na jamii yenye afya bora.
Kwa upande wake, Afisa Afya kutoka Halmashauri, Ndg. Cristiano Fusi, amesema kuwa zoezi hilo limekuwa la mafanikio kutokana na wananchi kuitikia wito wa kujitokeza kufanya usafi kwenye maeneo yao, lakini pia ametoa wito kwa wananchi, kuwa na desturi ya kufanya usafi mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa hatarishi pamoja na kuweka mazingira safi, badala ya kusubiri matamko kutoka kwa viongozi.
Kwa mwaka 2025, siku ya Usafishaji Dunian, hapa nchinii imeadhimishwa ikiwa na kauli mbiu inayosema, "Tunza Mazingira kwa Kuzipa Taka Thamani," ikiwa ina lengo la kuhamasisha jamii kwa ujumla juu ya namna bora ya udhibiti wa taka pamoja na kuwa na mazingira safi na salama.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa