Taaisi ya fedha, Benki ya CRDB, imekabidhi vifaa vya michezo zikiwemo seti za jezi pamoja na vifaa vya kufanyia mazoezi kwa Timu ya Netiboli ya vijana ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita katika juhudi za kuinua michezo kwenye Halmashauri.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana, Nyankumbu, Januari 4 ambapo yalitanguliwa na mechi ya kirakifiki baina ya timu hizo mbili, huku Timu ya Netiboli ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita ikiibuka kidedea kwa kushinda kwa magoli 41-16.




Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa