Muungano wa vikundi vilivyonufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mkoa wa Geita vimepeleka furaha kwa watoto yatima na walio na mazingira Magumu katika kituo cha Albayaan Islamic kilichopo ndani ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro.

Afisa Maendeleo ya jamii wa kata ya Katoro Lita Kelly Mwakaleja amesema vikundi hivyo vilivyotoa mikopo ni wanufaika wa mikopo ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita na vipo ndani ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro na ameiomba jamii kuiga mfano huo.

Nao baadhi ya wanavikundi walioungana wakitoka katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro ambao ni David Ezekiel Kalemela kutoka Ludete na Zephania Hosea kutoka kikundi Cha Mashujaa Katoro wakizungumza kwa niaba ya wenzao wamesema wameguswa na kutoa misaada hiyo kwa watoto hao ili kuwapatia faraja kuelekea kumaliza na kuukaribisha Mwaka mpya.
Mkurugenzi wa kituo hicho Shekhe Abobakar Nyerere ameshukuru kwa msaada huo uliowafikia watoto zaidi ya 60.

Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa