Watumishi wa umma wamesisitizwa kutambua vyema majukumu yao ya kazi ili waweze kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi.
Wito huo umetolewa na mratibu wa utawala na utumishi wa umma ofisi ya Rais Ikulu, Francis Mangira wakati akizungumza kwenye semina iliyofanyika katika ukumbi wa Gedeco ambayo imewahusisha watumishi wa umma wa Halmashauri ya wilaya na mji, Geita.
Pia Mangira amewataka watumishi hao kuepuka kuchanganya siasa na kazi ili kutoathiri utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Mratibu Msaidizi wa utawala na utumishi wa umma ofisi ya Rais, Ikulu Abdalah Mnongane amesema kila mtumishi anatakiwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo lakini pia kutofanya kazi kwa mazoea.
Aidha amewataka watumishi kuzingatia suala la maadili pia kuheshimu mamlaka, madaraka pamoja na mipaka ya majukumu yao ya kazi.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Geita Ali Kidwaka na Mkurugenzi wa mji mhandisi Modest Apolnary kwa pamoja wameahidi kuendelea kutekeleza maagizo mbalimbali ambayo yametolewa na waratibu hao kutoka ofisi ya katibu mkuu kiongozi, Ikulu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa