TImu za michezo mbali mbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita, zimeendelea kufanya vizuri baada ya kujinyakulia kombe la Mshindi wa Jumla Kimkoa kwa mara ya pili mfululizo kwenye Bonanza la Awamu ya Pili, ambapo ziliweza kuibuka kidedea baada ya kushika nafasi za kwanza kwenye michezo ya Riadha mita 100 na mita 200 (Wanaume), Netiboli, Kula (Wanaume), Karata (Wanaume), Kucheza Mziki, Kukimbiza Kuku, huku wenye mchezo wa Mpira wa Miguu, Timu ya Wanaume iliweza kushika nafasi ya pili.
Takribani taasisi 15 ziliweza kujitokeza kushiriki bonanza hilo siku ya tarehe 26, Julai katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana, Nyankumbu, likichagizwa na kaulimbiu iliyosema, “Michezo kwa Watumishi, Afya Bora na Ushirikiano Thabiti: Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025.”
Akifungua Bonanza hilo, Katibu Tawala (M) Geita, Ndg. Mohamed Gombati aliipongeza kamati ya maandalizi ya Bonanza hilo, huku akisisitiza kuwa nia na madhumuni ya bonanza hilo ni kujenga mshikamano, ushirikiano, pamoja na kudumisha mahusiano baina ya Watumishi pamoja na wananchi wa mkoa wa Geita.
Aidha, Ndg. Gombati pia aliwahimza watumishi na wananchi kwa ujumla kuwa na mazoea ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kupambana na magonjwa ya kisaikolojia ili kuboresha afya ya akili.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa