Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Halmashauri,Kata,Vijiji pamoja na Waandikishaji wapiga kura , Wametakiwa kufuata na kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma katika zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa ili kuepuka vurugu na kutoweka kwa amani katika uchaguzi huo.
Akizungumza katika Semina ya mafunzo elekezi ya uchaguzi wa serikali za mtaa iliyowahusisha wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata,kijiji,Halmashauri na waandikishaji wapiga kura ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Geita Ndugu,Ali Kidwaka amesema Halmashauri haitawavumilia wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi watakao enenda kinyume na taratibu na kanuni za uchaguzi.
Wakati huo hakimu mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Hakimu Kiiza Sostenes amewatahadharisha wasimamizi wasaidizi hao kutovunja kiapo walicho hapa kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na watachukuliwa hatua.
Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo elekezi wamesema uchaguzi wa mwaka huu wa Serikali za Mitaa unaishara ya utulivu na watazingatia sheria na miongozo ya uchaguzi.
Jumla ya wasimamizi wasaidizi 814 kutoka ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita wameshiriki katika semina hiyo elekezi iliyokwenda sambamaba na kula kiapo ikiwa ni Ishara ya kusimamia uchaguzi kwa haki na weledi katika uchaguzi wa serikali za mtaa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 Mwaka huu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa