Mafunzo kwa Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata, Halmashauri ya Waila ya Geita,yamefungwa leo Agosti 06, 2025 ambapo wameaswa kutunza Kiapo walichokula katika kusimamia uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.
Akizungumza wakati Kufunga Mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku tatu katika Ukumbi wa Bomani-Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Msimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Halmashauri Bi. Sarah Yohana amewaasa Wasimamizi hao kuepuka kutoa siri ambazo Tume haijawapa maelezo kuzitoa katika utekelezaji wa kazi zao.
Aidha Bi Sarah Yohana amewataka Wasimamizi hao kwenda kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo, wasimamizi wasaidizi wa vituo na makarani waongozaji wa wapiga kura ili kuwasaidia kusimamia zoezi la uchaguzi kwa weledi.
Pamoja na mambo mengine Bi Sarah amewataka kuandaa mafunzo hayo kwa kufuata usimamizi wao wa shughuli za kila siku za masuala ya uchaguzi.
Vilevile Bi Sarah amewahimiza Wasimamizi hao kubandika mabango, matangazo na orodha ya majina kwa kufuata kalenda ya utekelezaji wa majukumu ya uchaguzi ili kuepusha malalamiko ya ukiukwaji wa masharti ya sheria na kanuni za uchaguzi,
Pamoja na hayo Msimamizi huyo amesema katika uchaguzi huo kutakuwa na asasi na taasisi zilizopewa kibali kutoa elimu ya mpiga kura na kutazama uchaguzi hivyo amewakumbusha kuwa kazi ya waangalizi ni kutazama na si vinginevyo hivyo hawapaswi kusindikiza asasi au taasisi kwenye maeneo ambayo watayatembelea.
Katika Mafunzo hayo washiriki wameishukuru Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa namna ambavyo Mafunzo hayo yameendeshwa kwa weledi jambo ambalo litawafanya kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika zoezi la uchaguzi katika maeneo yao
Mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata, yalianza Agost 4 hadi agost 6 2025, yakiwa na jumla ya washiriki 74 kutoka katika kata 37 za Halmashauri ya Wilaya ya Geita huku yakibebwa na Kauli mbiu isemayo,” Kura yako Haki yako Jitokeze Kupiga Kura”
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa