Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Nzera ulioanza tarehe 5 Februari 2019 unatarajiwa kukamilika tarehe 30 juni 2019, hali itakayoboresha huduma za afya na kuhudumia takribani watu 825,600.
Kiasi cha pesa Tshs. 1,500,000,000/= kilipokelewa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo, ambapo OR-TAMISEMI ilitoa kipaumbele yajengwe majengo 7 ambayo ni Jengo la Utawala, Jengo la Wagonjwa wa Nje, Maabara, Jengo la Mionzi, Wodi ya Wazazi, Jengo la Ufuaji na Jengo la Kuhifadhia dawa.
Hospitali hiyo itakapokamilika itapunguza rufaa za wagonjwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Upatikanaji wa huduma kama vile mionzi, maabara kwa baadhi ya vipimo, uboreshaji wa huduma ya ufuaji, Upatikanaji wa huduma za dawa pamoja na huduma za wajawazito kujifungua.
Hata hivyo asilimia kubwa ya majengo hayo yapo kwenye hatua za mwisho za ukamilishaji(vigae, gypsum board na milango), na machache yapo kwenye hatua ya upauaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa