KATORO-GEITA
Wananchi Mkoani Geita wametakiwa kulinda amani na utulivu wakati Nchi inapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.
Hayo yamesemwa Mei 20, 2025 na Katibu wa Itikadi, Uenezi, na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla alipofanya Mkutano wa hadhara Katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
"Muendelee kulinda amani na utulivu kuelekea Uchaguzi ili Watanzania wapate haki ya kuchagua Viongozi wao." Amesema CPA Makalla.
Pamoja na hayo CPA Makalla amesema Mkoa wa Geita ni miongoni mwa Mikoa iliyofanya vizuri katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Vilevile Katibu huyo wa Itikadi, Uenezi, na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema Serikali inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amiri Jeshi Mkuu itaendelea kuwajali wachimbaji wadogo wakati na wakubwa ili kukuza uchumi.
"Adhma ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuwajali wachimbaji wa madini nchini ili kuendelea kukuza uchumi" Ameongeza CPA Amos Makalla.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Martine Shigela ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita kwa kutekeleza yale yote aliyo ahidi katika Mkoa wa Geita.
Mhe Shigela amesema katika Mkutano huo kuwa tayari Jimbo la Katoro limeshapatikana na sasa wananchi wanaomba upatikanaji wa Halmashauri baada ya Uchaguzi Mkuu .
Jimbo la Katoro limetokana na kugawanywa kwa Jimbo la Busanda na Kuifanya Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuwa na Majimbo matatu ya Uchaguzi ambayo ni Jimbo la Geita, Busanda na Katoro.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa