Wananchi wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro Halmashauri ya Wilaya ya Geita wametakiwa kuwa na bidii katika kuweka mazingira safi ili kuepuka Magonjwa ya milipuko.
Hayo yamesemwa Julai 26,2025 na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba aliposhiriki zoezi la kufanya Usafi Katika Mamlaka ya Mji huo wenye idadi kubwa ya watu.
"Tumekuja kushirikiana nanyi kufanya usafi eneo kwa eneo, kipande kwa kipande kwani tukicheka na uchafu, Mlipuko wa Magonjwa utatokea. Tunakata kulinda afya za watu kwani Usalama wa kwanza ni Afya ya Mtu" Amesema Mhe Komba
Aidha katika zoezi hilo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg.Karia Magaro amezitaka Kaya na Wafanyabiashara kuwajibika kutoa fedha kwa ajili ya kuzoa taka ili zisiendelee kuzagaa.
"Niwaombe wana Katoro kuwa tayari kuchangia ili fedha hizo ziweze kusaidia katika kuzoa taka ambazo zinazalishwa katika maeneo yenu" amesema Magaro.
Zoezi la Usafi limeshirikisha viongozi mbalimbali akiwepo Katibu Tawala wilaya ya Geita Bi Lucy Beda, kamati ya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Idara na Vitengo wakishirikiana na Wananchi wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa