Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Martine Shigela ameongoza wananchi wa Mkoa wa Geita katika Uzinduzi wa Maonesho ya Wiki ya Sheria ambayo yameanza tarehe 24-31,Januari 2025 katika viwanja vya EPZA vilivyo Geita.
Akiwa katika viwanja vya EPZA, Mhe Shigela ametembelea banda la Mahakama Kuu Kanda ya Geita,Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa( TAKUKURU), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii ( NSSF), Tume ya Usulihishi na Uamuzi(CMA), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Geita, Chama cha Mawakili wa kujitegemea, Madalali na Wasambazaji Nyaraka wa Mahakama.
Mabanda Mengine yaliyotembelewa ni banda la Uhamiaji , Magereza, Zimamoto na banda la wajasiriamali.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe Martine Shigela amewapongeza watendaji wa Mahakama kwa namna ambavyo wamejipanga kuifanikisha wiki ya sheria Mkoani Geita.
" Nimefarijika kuona washiriki wote wa Maonesho wamefika ili kuwahudumia wananchi na kuhakikisha Maonesho yanafana" Amesema Mhe Shigela.
Aidha Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kujitokeza katika viwanja vya EPZA ili kujifunza mambo mbalimbali ya kisheria.
" Tujitokeze kupata elimu, kupata ushauri wa kisheria ili kupata muongozo wa mambo mbalimbali ya kisheria kwani Mahakama ni chombo cha kutoa haki" Ameongez Mhe.Shigela.
Shigela Ameongeza kuwa malalamiko yanapopungua yanajenga heshima kubwa kwa Mahakama Kuu Kanda ya Geita.
Vilevile Mhe Shigela amepongeza matumizi ya Teknolojia kwa kurahisisha mahakama kufanya kazi kisasa
" Unaweza fungua mashauri kwenye mtandao popote pale ulipo ndani na nje ya nchi, pia nafarijika kuona utendaji na utoaji wa haki unaenda kwa wakati ndani ya mkoa wa Geita kwani kesi zimekuwa zikimalizika kwa wakati" Amesema Mhe Shigela.
Pamoja na hayo Mhe Shigela ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za mahakama na kuwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono mahakama kuu Kanda ya Geita.
"Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametia nguvu kuunga mkono kazi za Mahakama kwa kuleta kampeni ya Msaada wa Kisheria ijulikanayo kama Mama Samia Legal Aid Compaign (MSLAC) ambayo inaenda kusambaa katika vijiji Mkoani Geita" Amesema Mhe Shigela.
Maonesho hayo yamebebwa na Kauli mbiu isemayo: " Tanzania ya 2025, Nafasi ya Taasisi zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo"
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Martine Shigela akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya Sheria katika viwanja vya EPZA vilivyo Bombambili Manispaa ya Geita.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa