Na: Hendrick Msangi.
Jumla ya watahiniwa 47,286 wa darasa la nne wakiwemo Wavulana 22,531 na Wasichana 24,755 wameanza kufanya mitihani ya upimaji wa darasa la nne 2023 katika shule za msingi 234 Wilayani Geita.
Mkoa wa Geita una jumla ya shule za Msingi 742 zenye watahiniwa wa SFNA 2023 ambapo kati ya shule hizo , 690 ni za Serikali na 52 ni za binafsi.
Hilo ni ongezeko la shule 43 sawa na asilimia 6 ikilinganishwa na shule 699 zilizofanya mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la nne kwa mwaka 2022 katika Halmashauri 6 za Mkoa huo.
Akizungumzia maandalizi ya mitihani hiyo, Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndugu Paul R Magubiki amesema maandalizi yapo vizuri na semina zimetolewa kwa wasimamizi wa mitihani hiyo kwa shule zote ili mitihani hiyo iweze kufanyika katika ufanisi ulio kusudiwa.
“Semina zimefanyika kwa ufanisi kwa walimu wanaosimamia mitihani hii, kwani wameandaliwa vema kwa kufuata muongozo wa baraza la mitihani na vyombo husika vinavyounda kamati ya mitihani pia ulinzi na usalama upo wa kutosha, hivyo tunaamini watoto watafanya vizuri na tumewataka wasimamizi kuwaacha watoto kufanya mitihani hiyo wenyewe kwani ni mitihani ya upimaji tuweze kupata tathmini ya kile watoto walichojifunza kwa miaka minne” amesema Magubiki
Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nzera iliyoko kata ya Nzera Agustine Mabina amesema wanafunzi wamejiandaa vema kufanya mitihani hiyo ya upimaji wa kitaifa iliyoanza leo oktoba 25.
“Tumewaanda vema watahiniwa kwani wamefanya majaribio mengi ya mitihani ya ndani, mock Wilaya na mock Mkoa, pia tumewaanda kisaikolojia kufanya mitihani yao ya Upimaji wa Kitaifa, alisema Alisema Mabina.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Baraza la Mitihani la Tanzania imetoa ratiba ya kufanyika kwa mitihani ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne kwa siku mbili yaani Octoba 25 na 26, Aidha kwa upande wa wanafunzi wenye mahitaji maalum (wasioona, uoni hafifu , viziwi ), Wizara imeelekeza waongezewe muda wa ziada wa dakika 20 kwa kila saa kwa somo la Hisabati na dakika 10 kwa kila saa kwa masomo mengine na kuwepo kwa mtaalam mwaminifu wa mahitaji husika kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa