• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

WAGANGA WAKUU WAMTUNUKU RAISI TUZO, MHE. MPANGO AWAPONGEZA, ATOA MAELEKEZO MAHUSUSI

Posted on: July 13th, 2025

Na John Mapepele-DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo maalum ya kutambua mchango wake kwenye Sekta ya Afya na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri hii leo.

Tuzo hiyo ameitoa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Waganga hao na kumkabidhi Makamo wa Rais, Mhe. Dkt. Philipo Mpango aliyekuwa mgeni rasmi katika Mkutano huo wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri jijini Dodoma.

Mbali na tuzo hiyo pia Waganga Wakuu wamemtunukia Makamo wa Rais tuzo hiyo pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama.


Mhe. Mpango  amewapongeza Waganga Wakuu nchini kwa kazi wanayofanya ya kuwahudumia  wananchi huku akiwataka waendelee kuimarisha huduma na sekta ya afya kwa ujumla na kuzingatia maadili ya taaluma yao.

Amesisitiza kuwa Serikali itatekeleza mara moja maombi ya kuboresha stahili za wataalam hao kulingana hali halisi ya uchumi.

"Nawaelekeza Mawaziri wa Afya na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Waziri wa Fedha washughulikie suala la ucheleweshaji wa posho za madaktari na wahudumu wa afya." Amesisitiza Mhe. Mpango

Amesema kwa sasa Serikali inapoelekea kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa Wote Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatakiwa  kuhakikisha zinasimamia vema ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha yanatumika kiadilifu ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma.


Pia amewapongeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri/Manispaa na Majiji kwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo ile ya afya na vifaa tiba katika Halmashauri/Manispaa/Majiji.

Amesema ili kuimarisha huduma za afya na usimamizi shirikishi, Serikali imenunua na kusambaza magari ya kubeba wagonjwa (ambulance) na  mashine za kisasa za kidijiti (Digital X-ray na ultrasound) na kuagiza kuvitunza vifaa hivyo na vingine vitakavyonunuliwa ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.


Akimkaribisha Mhe. Mpango kutoa hotuba, Mhe.Mchengerwa amemshukuru Rais Samia kwa maono yake makubwa na miongozo kwenye sekta ya afya ambayo yameleta mapinduzi makubwa katika kipindi kifupi.

Mhe. Mchengerwa ametumia mkutano huo kutaja mafanikio lukuki yaliyopatikana katika kipindi hiki.

Aidha, amesema  mafanikio hayo pia yanatokana na ushirikiano baina ya Wizara yake na Wizara ya Afya.


Katika mkutano huo wadau mbalimbali ya afya pia wametunukiwa vyeti vya kutambua michango yao.

Tangazo

  • HIZI HAPA AJIRA ZA KUMWAGA GEITA DC July 15, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • GEITA DC YAANZA KWA KISHINDO SHIMISEMITA 2025, YACHAPA NETIBOLI, MPIRA WA WAVU NA SOKA!

    August 16, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA GEITA ATEMBELEA TIMU ZA HALMASHAURI SHIMISEMITA TANGA

    August 16, 2025
  • MORALI JUU: WACHEZAJI WA GEITA DC WAPANIA VIKOMBE VYOTE TANGA

    August 15, 2025
  • RAS-GEITA ATOA WITO WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025

    August 12, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa