Walenga mapya ni kikundi cha vijana sita ambao wameanzisha ufugaji wa samaki ndani ya Ziwa Viktoria katika eneo la Chanika Senga ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Wanapozungumzia Mradi huo wanasema kwamba, baada ya kufanya taratibu zote za kusajili Mradi wao,walianza ufugaji wa samaki kwa kuanzia na samaki 300 ambapo baadaye walizaliana na kufikia 1,500.
Leonard Ndalo ambaye ni kiongozi wa kikundi hicho cha Walenga Mapya, anaeleza kuwa katika kuwaendeleza kiuchumi,Halmashauri ya Wilaya ya Geita iliwapatia mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 6 na nusu, ambao waliutumia kuagizia vifaranga vya samaki takribani elfu 20, sambamba na kuboresha miundombinu ya mazingira ya ufugaji wa samaki ikiwemo kujenga maeneo maalumu, (Cages) za kutenganishia vifaranga na samaki wakubwa,ambapo mkopo huo marejesho yake yanaanza mwezi wa 11 mwaka 2021
Aidha Bw.Ndalo amesema miongoni mwa changamoto kubwa wanazokabiliana nazo ni pamoja na muindombinu duni ya kufaragua,huku wakiomba uwezeshwaji zaidi ili kukuza mradi huo.
Ameongeza kuwa malengo yao ya baadae ni kuzalisha na kuuza samaki angalau kwa kuanzia na tani 2 endapo mradi huo utaendelea kuboreka zaidi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa