Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga amewaondoa zaidi ya wachimbaji wadogo 2000 waliovamia jana katika mgodi wa Backleef uliopo kitongoji cha Mnekezi kata ya Lwamgasa.
Akizungumza na wachimbaji wadogo hao alisema kuwa eneo hilo ni la serikali na mapato yanayopatikana yanamfikia kila mwananchi hivyo waondoke kwa amani bila shuruti huku serikali ikiangalia namna ya wachimbaji wadogo kupata maeneo ya kufanya shughuli zao.
Ernest Maganga afisa madini mkazi mkoa wa Geita amesema kuwa eneo hilo lina leseni ya kampuni ya Backleef hivyo haipaswi wachimbaji wadogo kuingia na kufanya uchimbaji huo.
Wachimbaji wadogo kutoka maeneo mbalimbali walivamia eneo hilo kuanzia jana wakiwa takribani 150 hadi leo hii idadi yao ikaongezeka na kufikia zaidi ya elfu mbili.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa