Katika kuhakikisha elimu shirikishi juu ya kuendeleza miradi ya maendeleo kwa vikundi inakuwa na tija kwa walengwa,Vikundi vimeshauriwa kuwa na miradi endelevu ili kuzalisha na kupata faida kwa malengo waliojiwekea.
Mratibu wa mfuko wa wanawake Halmashauri Wilaya Geita Bi.Martha Mgina Akiwa Katika mafunzo ya pamoja na Vikundi vya wanawake,Vijana na Wanaume kata ya Katoro pamoja na Ludete juu ya matumizi sahihi ya fedha za mikopo na marejesho kwa wanavikundi amesisitiza wanavikundi kuwa makini pindi wapatapo fedha za mikopo na kuzitumia kwa malengo waliojiwekea.
Hata hivyo swala la utambuzi wa vikundi bado ni kitendawili kwani vikundi vingi havijasajiliwa na kukamilisha taratibu zilizowekwa hali iyowakosesha fursa ya kupata mikopo kwa wakati na kujiweka katika hatari ya kupoteza mitaji yao.
Fursa hii ya mikopo kwa Vikundi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeonekana kuchangamkiwa zaidi na wanawake tofauti na Vijana hali inayowalazimu watalaamu wa maswala ya mikopo kutoka taasisi ya fedha Benki ya Taifa ya biashara NBC kujitokeza na kuwashauri njia rafiki ya kutunza fedha kupitia akaunti zisizo na makato ili kulinda mitaji yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa mwaka wa fedha 2019/2020 imetenga zaidi ya milioni 351 kupitia mapato yake ya ndani ili kuvipatia vikundi kuendeleza miradi ya maendeleo katika mgawanyo wa wanawake 4%,Vijana 4% na walemavu 2% katika 10% zilizotengwa na Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa