Vijana katika mkoa wa Geita wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo hupatikana katika mkoa wa Geita ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Gabriel wakati akiongea na wafanyakazi wa RUBONDO FM Jumanne tarehe 28/08/2019 ambapo amesema Serikali ya awamu ya Tano ina fursa nyingi za kuwasaidia vijana.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Ali Kidwaka amewataka vijana wenye mipango ya maendeleo kujitokeza katika Halmashauri ili waweze kusaidiwa mitaji ya fedha.
Katika ziara hiyo fupi ndani ya ofisi ya kurushia matangazo Redio Rubondo Mhandisi Gabriel ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Geita kwa hatua kubwa ya kuanzisha redio ambayo ni fursa kubwa katika kuongeza mapato ya halmashauri.
Mhandisi Robert amesema kupitia ofisi yake na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita atajenga studio kubwa ya kisasa ya uzalishaji wa kazi za muziki ili kuongeza ufanisi wa urushwaji wa matangazo na usikivu mzuri.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa