Geita
Kamati ya Fedha uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Geita Januari 19, 2026 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jimbo la Geita.
Akizungumza katika ziara hiyo Diwani wa Kata ya Butobela Mhe Pascal Mapung’o amewataka Wahandisi wa Halmashauri kuhakikisha wanashughulikia kasoro zote ambazo zimeonekana kwenye miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutumika.
“Kasoro zote ambazo tumeziona kwenye miradi zifanyiwe kazi kwa wakati ili miradi ikamilike kwa wakati na kuanza kutumika” Amesema Mhe Mapung’o




Shule mpya ya Mchepuo wa Kiingereza Nzera Modern Pre & Primary School wenye thamani ya shilingi Milioni 573,791,319.36 kutoka CSR ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita. Shule hiyo imekamilika tayari kupokea wanafunzi
Aidha Mhe Mapung’o amewataka wasimamizi wa miradi kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Halmashauri ili miradi hiyo ikamilike kulingana na gharama zilizowekwa kwa kila mradi.
Naye diwani wa kata ya Chigunga Mhe Anthony Anacreti ametoa wito kwa viongozi wa kata na vijiji kuendelea kuwahamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo katika maeneo yao miradi inapotekelezwa.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Bi Sarah Yohana ambaye pia ni Afisa Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Geita amewataka mafundi ujenzi wanaotekeleza miradi hiyo kuongeza kasi ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati.




Ujenzi wa mradi wa shule ya msingi Kakubilo Madarsa 4 na matundu 6 ya vyoo Pamoja na ukarabati wa vyumba 8 vya madarasa na ofisi 2.Kukamilika kwake kutapunguza msongamano wa wanafunzi kwenye madarasa na kuweka mazingira safi ya kujisomea.
“Niwatake mafundi kuongeza kasi ya ujenzi ikiwa ni pamoja na wasimamizi wa miradi hii kuwalipa mafundi ujenzi kwa wakati” Amesema Bi Sarah
Vilevile Bi Sarah ametoa wito kwa Wasimamizi wa miradi kuwashirikisha wananchi katika maeneo yao utekelezaji wa miradi na kuwajulisha wananchi fedha za miradi zinapoingia ili wananchi waweze kushiriki kikamilifu miradi ya maendeleo.
Kamati hiyo ikiwa na wataalam kutoka Halmashauri, imetembelea miradi ya ujenzi wa shule, ukarabati wa miundombinu ya madarasa,ujenzi wa nyumba za watumishi Pamoja na uzio katika nyumba hizo miradi ambayo thamani yake ni kiasi cha Shilingi Bilioni 2.1.
Miradi hiyo ambayo imetembelewa na kamati ya fedha uongozi na mipango chanzo cha fedha ni Mapato ya ndani, BOOST na wajibu wa Kampuni ya mgodi wa dhahabu wa Geita kwa jamii (CSR-GGML)
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaendelea kuishukuru serikali inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za miradi, Pamoja na waheshimiwa wabunge kwa jitihada zao za kuleta maendeleo kwa wananchi wa Geita.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa