Vijana nchini wametakiwa kuwa mabalozi wa suala zima la uzalendo pamoja na kuhakikisha wanakua mfano bora kwa kuwa na maadili yanayohitajika kwenye jamii.
Akizungumza tarehe 1, Septemba wakati akifunga Kongamano la Vijana lililoratibiwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii na kujikita katika kutoa mafunzo mbali mbali kwa vijana katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ludete, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, 2025 Ndg. Ismail Ali Ussi, amewataka vijana waliohudhuria mafunzo hayo kuwa mfano wa kuigwa na wengine kwa kuwa na miyenendo yenye kuwa na maadili.
Ndg. Ussi pia amewahimiza vijana wenye sifa za kushiriki katika upigaji kura mnamo mwezi Oktoba, kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwa kuzingatia kwa kulinda tunu za Amani, Upendo na Utulivu.
"Twendeni tukashiriki uchaguzi mkuu kwa kuzingatia suala zima la amani pamoja na kuchagua viongozi wenye sifa. Raisi amejenga imani kubwa kwa wananchi kwa kutekeleza ahadi za serikali kwa vitendo." Amesema Ndg. Ussi.
Kongamano hilo lilihusisha mada zilizogusia masuala ya Uongozi na Maadili, Uzalendo na Uchaguzi, Ukatili wa Kijinsia, Haki na Wajibu, pamoja na kuwapatia vijana stadi mbali mbali za kazi, ambapo takribani vijana 425 (204 Ke, 221 Me) waliweza kuhudhuria kongamano hilo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa