Katika kuhakikisha dhamira ya kumtua mama ndoo kichwani inafikia malengo, Halmashauri ya wilaya ya Geita imekamilisha miradi ya maji safi na salama kwa wananchi waishio vijijini na miji midogo kwa kuongeza vyanzo vya upatikanaji wa maji.
Akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita Naibu waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso amepongeza jitihada za Halamshauri katika kufikisha huduma za maji safi na salama na kuwasihi wananchi kutunza na kulinda vyanzo vya maji ili kufikia lengo la kila kijiji kupata maji safi na salama.
Mhe.Aweso amesema miradi ya maji ni yenye gharama kubwa na serikali haitawavulia wahandisi na wakandarasi wote wanaotumika kuhujumu vyanzo vya maji, mpaka sasa wahandisi 67 tanzania wamesimamishwa kazi na wizara hiyo na makampuni 30 yamepelekwa bodi ya maji ili kufutiwa reseni
Naibu waziri huyo amesema Wizara imepokea fedha za mkopo nafuu kiasi cha Dola milioni 500 kitakachotumika katika katatua tatizo la maji Miji 28 Tanzania na Geita ikiwa miongoni,Wizara pia imeanzisha wakala wa maji vijijini LUWASA ili kusaidia kwa karibu utendaji katika sekta ya maji Tanzania.
Halmashauri ya Wilaya Geita imetekeleza Miradi mikubwa ya maji, mradi wa Chankorongo uliogharaimu zaidi ya Bilioni 4.9 umekamilika na wananchi wananufaika lakini pia mradi wa maji kisima cha maji Luhuha kata ya nyakagomba ambao umetengewa zaidi ya milioni 600 na umefikia katika hatua za mwisho
Utayari wa wananchi kutumia vyanzo halali vya maji na sio vyanzo vya asili vya maji kama visima imeonekana bado ni kitendawili hasa vijijini hali inayopelekea miradi ya maji kushindwa kujiongoza kutokana na gharama kubwa za uendeshwaji wa miradi hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa