Katika kuhakikisha miundombinu ya Elimu inaboreshwa na kuongeza chachu ya ufaulu kwa wanafunzi hasa ndani ya Halmsahauri ya Wilaya ya Geita, ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya kidato cha Tano na Sita katika Shule ya sekondari Bugando kata ya Nzera umefikia katika hatua nzuri.
Katika mpango huo vyumba vya madarasa vitano tayari vimejengwa vinayoweza kuchukua wanafunzi wa michepuo mitatu tofauti na kuwa shule ya sekondari ya kwanza kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kufikia hatua hiyo.
Mbali na ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa ukarabati wa mabweni mawili ya wavulana katika shule hiyo unaendelea chini ya mpango wa Halmsahauri, fedha ya CSR kutoka Mgodi wa dhahabu wa Geita GGM pamoja na fedha za jimbo la Geita Vijijini.
Kwa upande wa taaluma Mkuu wa shule ya sekondari ya Bugando Bwana,William Wanche amesema kukamilika kwa ujenzi huo utaongeza ufanisi na chachu ya maendeleo ya elimu na ufaulu kwa kata hiyo kutokana na mchanganyiko wa wanafunzi watakao toka nje ya Mkoa wa Geita kuja kusoma katika shule hiyo.
Katika hatua nyingine za kusaidia jitihada za kutekeleza malengo ya milenia ya maendeleo endelevu,hususani lengo namba 3 la Afya Bora na Ustawi wa Watu, Halimashauri ya Wilaya Geita ikishiarikiana na mpango wa maendeleo CSR imendelea kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya kila kata na Zahanati Kila kijiji ili kuongeza ufanisi katika sekta ya afya.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa