Mkuu wa Mkoa Geita alidhishwa na ujenzi wa Sekondari ya Ghorofa.
Mkuu wa mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel, amependezwa na ujenzi wa shule ya ghorofa ya sekondari Nyalwanzaja iliyopo Halmashauri ya Wilayani Geita ambayo itaondoa changamoto ya wanafunzi kutembea zaidi ya KM 14 kufuata elimu.
Mradi huo wa shule ya ghorofa umeambatana na ujenzi wa nyumba pacha ya walimu pamoja na matundu kumi ya vyoo unagaharimu zaidi ya Milioni 200.
Mhandisi Gabriel amesema shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu za wananchi, halmashauri pamoja na wadau itakua shule ya kwanza ya Ghorofa Geita itakayo jumuisha kidato cha tano na sita
Aidha Mkuu wa Mkoa ameridhishwa na matumizi ya fedha yaliyotumika kwenye ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Buyagu mradi uliogharimu shilingi Milioni 90.
Shule hiyo tayari imejengwa madarasa 5, Ofisi 2 za walimu na matundu 8 ya vyoo na madarasa mengine mawili yakiwa kwenye hatua ya boma.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa