Awamu ya kwanza ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura, umeweza kutamatika Wilayani Geita hapo Jana, huku ukishuhudia idadi kubwa ya watu, hususani kundi la vijana likijitokeza kujiandikisha kwenye zoezi hilo.
Zoezi hilo lililodumu kwa muda wa wiki moja toka Mei Mosi, liliweza kushuhudia vituo takribani 44 vya Uboreshaji wa daftari hilo ndani ya kata zote 37, ambapo jumla ya wananchi 93,523 walijitokeza kwenye zoezi hilo.
Hatua hii ni sehemu muhimu ya maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika badae Mwezi Octoba mwaka huu, huku ukiweka msingi thabiti kwa ushiriki mpana wa wananchi katika mchakato wa kidemokrasia na kuongeza muamko wa kisiasa kwa makundi mbali mbali wakiwemo vijana, wanawake na wazee.
Kukamilika kwa zoezi hili kunatarajiwa kufuatiwa na uchakataji wa taarifa na uhakiki wa takwimu kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kabla ya hatua zinazofuata kutangazwa hapo badae.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa