Wananchi wa Kata ya Katoma jimbo la Geita wametakiwa kuilinda amani ya nchi ya Tanzania kwa wivu mkubwa huku wakitakiwa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama kwa wale wote wanaojihusisha na matukio ya kiuhalifu.
Hayo yamesemwa Septemba 23, 2024 kwenye mkutano wa Hadhara ambapo Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba ameseikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa kata hiyo.
“Amani ikivurugika hakuna maendeleo, pigeni vita uzushi mbalimbali unaoendelea maeneo tofauti ikiwa ni pamoja na taarifa za watu kung’olewa figo pamoja na wale wote ambao wanarudisha maendeleo ya watu wakiwepo vibaka, wezi na waporaji ili tujenge jamii yenye amani na utulivu” Amesema Mhe Komba.
Pamoja na hayo Mhe Komba amewasihi wananchi wa Kata hiyo kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupokelewa Octoba 05, 2024 na kukimbizwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Mhe Hashim Komba Mkuu wa wilaya ya Geita amewataka wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kutoa elimu kuhusu mikopo inayotolewa na Serikali ili wananchi wanufaike na mikopo hiyo isiyokuwa na riba.
“Mwenge wa uhuru unakuja kuchochea shughuli za maendeleo katika maeneo yetu hivyo tujitokeze” amesisitiza Mhe Komba.
Katibu Tawala Wilaya ya Geita Bi Lucy Beda akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kata ya Katoma Septemba 23, 2024.
Aidha Mhe Komba amewataka wananchi hao kijitokeza kuanzia tarehe 11 hadi 20 Octoba kwenda kujiorodhesha kwenye daftari ili kupata nafasi ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Karia Rajab Magaro Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita akiwahimiza Wananchi kujitokeza kijiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Wananchi wa Kata ya Katoma wakifuatilia Mkutano wa Hadhara Septemba 23, 2024 ambapo wametoa kero mbalimbali zinazowakabili na kupatiwa ufumbuzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa